arrow_back
All Announcements
weekly
Matangazo ya Kanisa 18 – 24 MEI 2026
calendar_today
May 15, 2026
person
Super Admin
picture_as_pdf
Attachment Available
3opTwfRJo76boGjXvjeC8UqhmCRmFyxrf8hJOfvN.pdf
VIONGOZI WA ZAMU
18 –24 MEI 2026
MCHUNGAJI
REV. BRYSON KITOI 0755 641 497
MZEE WA KANISA:
MCH. GREYSON NYANTAMBA
WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU
WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI
SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE
24/05/2026:
MR. RODERICK LUTEMBEKA
MR. REMIGIUS NGAIZA
MRS. THERESIA MWABUSILA
MASHEMASI WA ZAMU:
MR. EGIDI PATRICK
MRS. EMMA BENJAMIN
MRS. FLOTEA MASSAWE
MR. FABIAN QWARAY
ZAMU ZA WATENDAJI
Watendaji wote wa kundi la BETHLEHEMU mtakuwa
zamu ya mfungo na maombi siku ya Jumamosi ijayo ya
tarehe 23/05/2026.
Watendaji wote waliopo maeneo ya
Mzee Remigius Ngaiza, Mrs Rhoda Bundara, Mzee
Greyson Nyantamba na Dr. Dickson Mkoka.
TANGAZO
1. Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa
kutembelea vituo vyenu vya HBCF ili kujua
maendeleo ya vituo hivyo na kuviimarisha,
wakisaidiana na makatibu pamoja na
mashemasi.
2. Kutakuwa na Ibada ya shukrani ya nusu mwaka pamoja na Ushirika wa meza ya Bwana
tarehe 28.06.2026. Washirika wote tujiandae
na ibada hiyo yenye baraka.
MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI
1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango
wa ujenzi kwa awamu hii ya sita kutoa au kupunguza
ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendelee, mwisho wa
kuchangia awamu hii ni mwezi Januari 2026.
Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako
na kwa vizazi vyako.
2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:
015 0020374000 CRDB BANK.
Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH
PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU
TANGAZO IDARA YA WATOTO
1. Tarehe 30.05.2026: Huduma ya kutembelea
gereza la watoto Upanga kuanzia saa mbili
asubuhi, gharama ya usafiri kwa kila mtoto ni
Tzs. 2,000 pamoja na sadaka ya ukarimu.
2. Tarehe 13.06.2026 : Mkesha wa kusifu na
kuabudu, maombi na kuonyesha vipaji
3. Tarehe 15– 21 Juni 2026 wiki ya Idara ya watoto na wanafunzi, kutakuwa na makambi
hapa kanisani kuanzia saa 8 mchana hadi saa
12 jioni
4. Ibada ya Jumatano na Ijumaa (HBCF) zitaongozwa na Idara ya watoto.Njoo na familia
yako yote upokee kutoka kwa Bwana.
5. Tarehe 21.06.2026 ni kilele cha sikukuu ya
watoto, sare ziko tayari (Tshirt) bei ni Tzs
10,000.
SEMINA YA UAMSHO KWA KANISA
ZIMA
Kutakuwa na semina ya uamsho kuanzia tarehe
24– 31 Mei 2026.Kila mshirika ajiandae kuinuliwa kiroho, kiuchumi, kibiashara kupitia semina
hiyo. Kwaya zote , Praise team pamoja na idara
ya maombi zijiandae.