arrow_back
All Announcements
weekly
Matangazo ya Kanisa 25 – 31 MEI 2026
calendar_today
May 24, 2026
person
Super Admin
picture_as_pdf
Attachment Available
klGegyva5oWWEvk2Rk2uCj1pKvoZBGU7AA3cvvC8.pdf
VIONGOZI WA ZAMU
25 –31 MEI 2026
MCHUNGAJI
REV. JOSEPH ENOS 0755 641 497
MZEE WA KANISA:
MCH. YOTHAM MACKENZIE
WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU
WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI
SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE
31/05/2026:
MRS. THERESIA MWABUSILA
MR. MATHIAS MSANGI
MR. JOSEPH MAMUYA
MASHEMASI WA ZAMU:
MR. FRANCES MASSAWE
MR. GEORGE WANDWALO
MISS. GLORY MARTIN
MRS. GRADES EDGAR
MATANGAZO
Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea
vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo
hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu
pamoja na mashemasi.
Kutakuwa na Ibada ya shukrani ya nusu mwaka pamoja na Ushirika wa meza ya Bwana tarehe 28.06.2026.
Washirika wote tujiandae na ibada hiyo yenye baraka.
Mchungaji kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae
zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson
Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri
chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba.
MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI
1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango
wa ujenzi kwa awamu hii ya sita kutoa au kupunguza
ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendelee, mwisho wa
kuchangia awamu hii ni mwezi Agosti 2026.
Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako
na kwa vizazi vyako.
2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:
015 0020374000 CRDB BANK.
Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH
PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU
TANGAZO IDARA YA WATOTO
1. Tarehe 30.05.2026: Huduma ya kutembelea
gereza la watoto Upanga kuanzia saa mbili
asubuhi, gharama ya usafiri kwa kila mtoto ni
Tzs. 2,000 pamoja na sadaka ya ukarimu.
2. Tarehe 13.06.2026 : Mkesha wa kusifu na
kuabudu, maombi na kuonyesha vipaji
3. Tarehe 15– 21 Juni 2026 wiki ya Idara ya watoto na wanafunzi, kutakuwa na makambi
hapa kanisani kuanzia saa 8 mchana hadi saa
12 jioni
4. Ibada ya Jumatano na Ijumaa (HBCF) zitaongozwa na Idara ya watoto.Njoo na familia
yako yote upokee kutoka kwa Bwana.
5. Tarehe 21.06.2026 ni kilele cha sikukuu ya
watoto, sare ziko tayari (Tshirt) bei ni Tzs
10,000.
TANGAZO LA NDOA
Kwa mara ya kwanza tunatangaza harusi kati ya
kaka Jovin Jonathan Jovitha na dada Emiliana
Bruno Kipeto wote ni washirika wa TAG Kinondoni .Harusi itafanyika siku ya Jumapili tarehe
14/06/2026 hapa kanisani TAG Kinondoni.