MATANGAZO YA WIKI 13—19 JULAI 2026
arrow_back All Announcements
weekly

MATANGAZO YA WIKI 13—19 JULAI 2026

calendar_today July 11, 2026 person Kinondoni Revival Church
picture_as_pdf

Attachment Available

13-19-july-2026_20260711_102042.pdf

download Download PDF

VIONGOZI WA ZAMU

13—19 JULAI 2026

MCHUNGAJI MCH. WITNESS SWAI 0629 534 530

MZEE WA KANISA: MCH. YOTHAM MACKENZIE

WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE 19/7/2026:

MRS. THERESIA MWABUSILA

MR. MATHIAS MSANGI

MR. JOSEPH MAMUYA

MASHEMASI WA ZAMU:

MR. STEPHANO KAYANA

MISS. TATU HAMISI

MR. TIMOTH ANDERSON

MRS. VICKY ALFAKSA

MATANGAZO

Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu pamoja na mashemasi.

Mchungaji Kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba.

MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI

1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango wa ujenzi kwa awamu hii ya sita B kutoa au kupunguza ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendele. Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako na kwa vizazi vyako.

2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:

015 0020374000 CRDB BANK.

Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH

PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU

ZAMU ZA MAOMBI YA WATENDAJI

Watendaji wote wa kundi la BETHLEHEMU mtakuwa zamu ya mfungo na maombi siku ya Jumamosi ijayo ya tarehe 18/07/2026. Watendaji wote waliopo maeneo ya Mzee Remigius Ngaiza, Mrs Rhoda Bundara, Mzee Greyson Nyantamba na Dr. Dickson Mkoka.

MKUTANO MKUBWA WA INJILI

Kutakuwa na Mkutano mkubwa wa Injili katika viwanja vya Mwananyamala kwa Kopa kuanzia Tarehe 23—30 August. Washirika wote tunahimizwa kuuombea Mkutano na pia tujipange kushiriki kikamilifu kwa siku zote nane (8) .

TANGAZO LA NDOA

Kwa mara ya pili tunatangaza harusi kati ya kaka Elias John Songa wa TAG Kinondoni na dada Mariana Paul Martin wa Jerusalem Temple Geita Harusi itafanyika Jumapili tarehe 26/07/2026 hapa kanisani TAG Kinondoni.