MATANGAZO YA WIKI 03 - 09 AGOSTI 2026
Attachment Available
03-09-aug-2026_20260801_190221.pdf
VIONGOZI WA ZAMU AUGUST 2026
MCHUNGAJI
MCH. WITNESS SWAI 0629 534 530
MZEE WA KANISA
MR. MATHIAS MSANGI
WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE 09/8/2026
MCH. YOTHAM MACKENZIE
MCH. DICKSON MKOKA
MR. JOSEPH MAMUYA
MASHEMASI WA ZAMU
MRS. BEATRICE MLIMBILA
MR. CASTORY KUTIKA
MR. CLEMENT ZONGELA
MR. CHRISTIAN CHARLES
MATANGAZO
Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu pamoja na mashemasi.
Mchungaji Kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba.
Tarehe 07/08/2026 yaani Ijumaa ijayo, Kutakuwa na mkesha wa vijana wote katika Section Yetu ya Kijitonyama, ambao utafanyika hapa TAG Kinondoni. Hivyo: vijana wote mnahimizwa kushiriki mkesha huo.
MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI
1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango wa ujenzi kwa awamu hii ya sita B kutoa au kupunguza ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendele. Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako na kwa vizazi vyako.
2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:
015 0020374000 CRDB BANK. Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH
PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU
ZAMU ZA MAOMBI YA WATENDAJI
Watendaji wote wa kundi la YERIKO mtakuwa zamu ya mfungo na maombi siku ya Jumamosi ijayo ya tarehe 08/08/2026. Watendaji wote waliopo maeneo ya Mch Bryson Kitoi, MrsNatujwa Winzah, Mr. Mathias Msangi na Dr. Christian Mollel.
MKUTANO MKUBWA WA INJILI
Kutakuwa na Mkutano mkubwa wa Injili katika viwanja vya Mwananyamala kwa Kopa kuanzia Tarehe 30 Augusti hadi 06 Septemba 2026 Washirika wote tunahimizwa kuuombea Mkutano na pia tujipange kushiriki kikamilifu kwa siku zote nane (8)
TANGAZO LA NDOA
Kwa mara ya pili tunatangaza harusi kati ya kaka Anyitike Enock Mwangungulu na dada Fortunata Gideon Patrick wote ni washirika wa TAG Kinondoni Harusi itafanyika siku ya Jumapili tarehe 26/08/2026 hapa kanisani TAG Kinondoni.
MABADILIKO YA RATIBA YA CMF
Ibada ya CMF hapa kanisani kwa sasa itaanza kuanzia saa 12 jioni hadi saa 1 usiku ni maombi, saa 1 usiku hadi saa 2 usiku ni neno la Mungu. Wanaume wote mnahimizwa kushiriki.